Kituo cha Alkafeel cha taaluma na utafiti chatengezeza ramani tatu (3) zinazo onyesha barabara kuu zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala…

Maoni katika picha
Katika juhudi zake za kuandaa mwongozo wa mazuwaru na wakazi, kituo cha Alkafeel cha taaluma na utafuni chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetengeneza ramani tatu (3) zinazo onyesha njia kuu zinazo ingia katika mji wa Karbala, ramani hizo zinaonyesha maeneo ya kupata huduma za afya, vituo vya usalama, miji mikubwa na midogo, na zimeonyesha kwa kutumia namba alama zilizopo katika barabara hizo, kwa kutokea Najafu, Bagdad na Hilla.

Mkuu wa kituo hicho, Ustadhi Jasaam Muhammad Saidiy amesema kua: “Kazi ya kukusanya taarifa kwa ajili ya kuandaa ramani hizo na kuzichora ilidumu kwa miezi miwili takriban”.

Akaongeza kusema kua: “Tumechapisha nakala nyingi za ramani hizi katika saizi mbili (6*3) na (3*1.5) kila barabara inaramani yake rasmi, sehemu ndogo ya ramani hizo zimewekwa katika vibanda vya walio potelewa vilivyopo katika njia hizo, vinavyo simamiwa na idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi, katika ramani hizo kumechorwa alama inayo muelekeza zaairu sehemu ya kusimama, na zimeandikwa kwa lugha nne (4) Kiarabu, Kiurdu, Kifarsi na Kiengereza, huku idadi kubwa ikiwekwa katika vituo vikuu vya kutoa huduma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: