Tukiwa katika kutekeleza majukumu yetu ya kutangaza harakati za mazuwaru wanao kwenda Karbala kwa miguu kutokea Najafu, tuliona maukibu iliyo zungukwa na mawakibu nyingi za watoa huduma zilizo jaa katika barabara hii, maukibu hiyo ilikua na pendera nyingi za nchi za kiislamu, kiarabu na kiajemi, walikua na kitambaa kikubwa kilicho andikwa (Maukibu ya Arubainiyya ya wa Afrika wapenzi wa Hussein), tukavutiwa kuingia katika maukibu hiyo, tukakuta jopo la watu wanatoa huduma, lakini sio huduma kama zilizopo katika mawakibu zingine za kugawa chakula na maji hapana, tulikuta wameweka meza zikiwa zimezungushiwa viti, na katika kila meza kuna alama inayo onyesha lugha anayo tumia mtoa huduma aliyopo katika meza hiyo.
Tulipo fika hapo, tulikaribishwa na mmoja wa wasimamizi wa maukibu hiyo ambaye ni muafrika kutoka (Brokinafaso) anaitwa (Saidi Sanko) anaongea kiarabu, akatuelezea kuhusu maukibu hiyo na huduma wanazo toa, akasema kua: “Maukibu hii inafanyika kwa mwaka wapili, lakini mwaka huu imekua kubwa kushinda mwaka jana, na imeundwa kupitia mialiko mbalimbali tunayo peana wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) kutoka nchi mbali mbali kwa kutumia mitandao ya kijamii, ndipo tukapata wazo la kuanzisha maukibu ya kitamaduni itakayo sambaza fikra na malengo ya muhanga wa Imamu Hussein (a.s) kwa mazuwaru wageni wanao kusudia kuja katika ziara ya Arubaini, na watafikisha ujumbe kwa kutumia lugha zao, na hii maukibu inakua ndio inayo waunganisha watu wa mataifa mbalimbali chini ya mapenzi ya Hussein”.
Akaongeza kusema kua: “Maukibu hii inawawakilishi kutoka nchi (30), na wala sio nchi za Afrika peke yake, imeitwa kwa jina hili kwa sababu waanzilishi wake walikua ni wa Afrika wapenzi wa Imamu Hussein (a.s), hapa tunajibu maswali ya mazuwaru na tunatoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo wanayo hitaji kufahamu kuhusu Imamu Hussein (a.s) na kuhusu huduma zinazo tolewa na wairaq kwa mazuwaru pamoja na kuonyesha picha za viongozi wakubwa katika ulimwengu wa kiislamu walio fuata nyayo za Imamu Hussein (a.s)”.
Sanko akabainisha malengo ya maukibu kua ni: “Kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) kwa walimwengu kupitia mazuwaru wao, vile vile tuna angalia namna ya kufanya kwa wale ambao wamefanyiwa dhulma, wamenyanyaswa na kuadhibiwa kwa sababu tu ya kumpenda kwao Imamu Hussein (a.s), na tunaunda umoja na mshikamano kwa waumini wa dini zote na madhehebu zote kwa sababu Imamu Hussein (a.s) hakukusudia watu wa dini fulani au madhehebu au taifa, bali alikusudia kuwakomboa wanadamu wote, kutokana na haya tunatarajia tupate sifa ya kua watumishi wa kimataifa wa Imamu Hussein”.
Akasema: “Kila mshiriki wa maukibu hii ataelezea hali ya nchi yake au mataifa yanayo ongea lugha yake kuhusu alicho pata katika njia hii tukufu ya Imamu Hussein (a.s)”.
Katika kumalizia, Sanko akasisitiza kua: “Sisi ni wawakilishi wa nchi tofauti, hatuja wahi kuona wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) walio ingiza mapenzi hayo katika mwenendo (maisha) yao kama walivyo wairaq, huu ndio ukweli yapasa usemwe, na uigwe na mataifa mengine duniani, kwa sababu ya mapenzi yao makubwa kwa Hussein wamekumbwa na shari za madhwalimu wanaojaribu kuwaua na kuwadhofisha, hongera sana kwa wairaq kwa kudumu katika mapenzi haya”.