Shirika la usalama Alkafeel lafungua zaidi ya vituo 300 vya kutoa huduma ya kupiga simu bure…

Maoni katika picha
Miongoni mwa malengo yao ya mwaka katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), shirika la usalama Alkafeel limefungua zaidi ya vituo (300) vya kutoa huduma ya kupiga simu bure, vituo hivyo vimesambazwa sehemu mbalimbali katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru watukufu, bila kusahau vituo vilivyopo katika makao makuu ya miji, huduma hii imetoa fursa kwa mazuwaru wenyeji au wa kigeni kupiga simu bure katika mtandao wowote ule, wa kitaifa au kimataifa.

Pamoja na vituo hivi, kuna vituo vya walio potelewa, vilivyo jaa katika mji wa Karbala na Najafu pamoja na katika barabara zinazo unganisha miji hiyo, navyo vinatoa huduma hii pia.

Makamo rais wa kituo cha uongozaji walio potea Muhandisi Husaam Muhyi-Dini amesema kua; vituo vya kupiga simu bure vilivyo wekwa na shirika la usalama la Alkafeel kwa mwaka wa kumi mfululizo, vina msaada mkubwa kwa kituo cha kuongoza walio potea, kwani kinaweka mazingira salama zaidi kwa kupiga simu za ndani na nje ya Iraq.

Shirika hilo limetengeneza mitambo mizuri inayo saidia kupata mawasiliano bora ya simu bila kukata kata sauti, jambo ambalo hutokea wakati mwingine kutokana na kuzidiwa kwa mtandao, huduma hii imewafurahisha sana mazuwaru, na wameweza kuwapigia simu ndugu na jamaa zao, au kwa ajili ya kujiridhisha kuhusu mtu aliye potea au anaye tafutwa.

Kumbuka kua moja ya huduma za vituo vya kupiga simu bure ni kuhakikisha usalama wa mtandao wa mawasiliano ya bure katika vituo vya waliopotelewa vilivyo chini ya Atabatu Alawiyya tukufu na vile vya Atabataini (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu, pamoja na kutoa fursa kwa mazuwaru waendao Karbala kuwapigia simu ndugu na jamaa zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: