Atabatu Abbasiyya yakanusha taarifa ya kukusana sadaka kwa ajili ya kuwalisha mazuwaru na kunufaisha taasisi zake…

Maoni katika picha
Baadhi ya mitandao ya kijamii hivi karibuni imesambaza habari kutoka katika chombo cha habari cha Iran, ikisema kua Atabatu Abbasiyya tukufu inakusanya sadaka kwa ajili ya kuandaa chakula cha mazuwaru wa Arubaini, na inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru katika kipindi hiki cha ziara ya Arubaini, katika maukibu ya Ataba mbili tukufu kwenye barabara ya Najafu!!!.

Katika tamko lililo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu limekanusha taarifa hii ya uongo, isiyo kua na ukweli wowote, na iko mbali sana na mwenendo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Wamebainisha kua; huduma zote wanazo toa kwa mazuwaru kupitia maukibu ya Ataba mbili tukufu au majengo yake ya huduma ni bure kabisa, hawana uhusiano na mtu yeyote anaye kusanya michango au sadaka, mtu yeyote atakaye kusanya kwa jina leo ni muongo.

Na wametoa tahadhari kwa wananchi na mazuwaru watukufu ya kutomuamini mtu yeyote atakae kusanya michango.

Na wametoa wito kwa wananchi na mazuwaru watukufu kuto toa ushirikiano wowote kwa mtu wa aina hiyo, na badala yake waijulishe Ataba haraka, na wameiambia mitandao ya kijamii kua na tahadhari katika kusambaza ujumbe wa aina hiyo, habari yeyote kuhusu Atabatu Abbasiyya waichukue katika mitandao yake rasmi na vyanzo vyake vya habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: