Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji chatumia askali wake elfu tatu kuwalinda mazuwaru wa Arubaini na chatoa huduma kwao…

Maoni katika picha
Kama kawaida yake katika kila msimu wa ziara, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimeimarisha ulinzi kwa mazuwaru wa Arubaini kwa kusambaza askali elfu tatu (3000) katika njia zinazo ingia Karbala, pamoja na kutoa huduma kwa mazuwaru hao.

Wamekuja kushiriki katika kazi hii baada ya kupata ushindi dhidi ya makaidi wa Daesh katika vita ya kukomboa mji wa Qaaim, na kuwasiliana na kamanda wa kikosi cha Furat pamoja na kamanda wa mkoa wa Karbala, kimeweka askali wake katika barabara kuu tatu (Karbala – Baabil, Karbala – Bagdad na Karbala – Najafu), pia wapiganaji wengine wamevaa nguo za kiraia na wanachanganyika na mazuwaru ili muchunguza mienendo ya mazuaru na kudhibiti kwa haraka tatizo lolote linalo taka kutokea katikati ya makundi ya watu.

Pia wanashiriki katika sekta ya kutoa huduma kwa mazuwaru, wamefungua kituo cha afya na wanatoa misaada na maelekezo kwa mazuwaru, miongoni mwa wapiganaji hao wapo walio hitimu mafunzo katika vituo vilivyo funguliwa na kikosi hiki kila mkoa, ikiwa kama sehemu ya kutekeleza agizo la Marjaa dini mkuu, alipo sema kuhusu umuhimu wa kuandaa raia wa aina zote kwa ajili ya kupambana na hatari yeyote inayo weza kutokea katika nchi hii, kwa hiyo walikua kama wanajeshi wa hakiba wa kikosi hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: