Hospitali ya rufaa Alkafeel yasambaza vituo vya afya kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru watukufu…

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel katika mkoa wa Karbala, imetangaza kushiriki katika kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru wanao shiriki katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa kuweka vituo vya afya vyenye madaktari na wauguzi mahiri wa kiiraq na kigeni wanao shiriki katika kutoa huduma hiyo ya matibabu.

Kiongozi mkuu wa hostitali hiyo dokta Haidari Bahadeli amebainisha kua: “Vituo vyetu vya afya vimewekwa katika maeneo tofauti ndani ya mji wa Karbala na katika njia za watembea kwa miguu kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Vituo vyetu vilianza kutoa huduma toka walipo anza kuwasili wageni katika mji wa Karbala mwezi kumi Safar, na vitaendelea kutoa huduma hadi baada ya ziara ya Arubaini, tunatoa matibabu kwa mazuwaru na wenye hali mbaya tunawapeleka katika hospitali ya rufaa Alkafeel au katika hospitali zingine, tuna madaktari bingwa wa kiiraq na kipakistani pamoja na kutoka katika nchi zingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: