Ewe mpenzi wa Hussein unapo ingia Karbala kwa ajili ya kumzuru bwana wa mashahidi kumbuka…

Maoni katika picha
Hakika aridhi hii ndio alipo uawa mjukuu wa Mtume na watoto wake na maswahaba wake, hakika ni aridhi ambayo ilimwagika damu takasifu na wakachukuliwa mateka wanawake bora.

Fahamu katika moyo wako utukufu wa aridhi hii, udongo wake ni ponyo, wala hakataliwi mwenye kuomba, Mwenyezi Mungu ameifanya aridhi hii kua bora miongoni mwa aridhi za peponi, iingie kwa utulivu na unyenyekevu.

Tafakari katika nafsi yako, kipenzi wako Hussein kasimama na wanamfuata wafuasi wake na kumuomba ruhusa ya kuingia katika jihadi, wakisema: Amani iwe juu yako ewe Abu Abdillahi, na akawaruhusu, wakapigana na kupata shahada hadi akabakia mmoja miongoni mwao, naye akajitosa katika mapigano ili naye ajitolee nafsi yake tukufu, hebu kariri na wewe katika moyo wako na ulimi wako (Laiti ningekua pamoja na nyie nikafaulu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: