Kwa ajili ya kuongoza mazuwaru: Kitengo cha utumishi chasambaza idadi kubwa ya waelekezaji ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa mpango wake katika ziara ya Arubaini, kimesambaza waelekezaji ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kwa ajili ya kuwaelekeza mazuwaru sehemu wanazo taka kwenda.

Kitengo kimeandaa jopo la watumishi na kuwapa jukumu hilo pamoja na kuwaongezea nguvu kwa kuwapa watumishi wa kujitolea kwani wanafanya kazi saa 24, na wanayapa umuhimu zaidi maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu, wanawaelekeza mazuwaru sehemu za milango ya wanaume na wanawake pamoja na sehemu za vituo vya kutoa huduma zilizo andaliwa na Ataba tukufu, kama vile; mabanda ya walio potelewa, mabanda ya kuweka vifaa (amanaat), sehemu za kuweka viatu, sehemu za kulala, sehemu za matangazo na mengineyo.

Hali kadhalika wanajukumu la kutoa taarifa kwa kikosi cha uokozi itakapo tokea hatari yeyote, pia wanajukumu la kumchukua aliye potea au potelewa na kumpeleka sehemu husika, asilimia kubwa ya mazuwaru kutokana na kutembea kwa muda mrefu wana uchovu mkubwa unao sababisha kupungua kwa umakini wao, hivyo watu hawa wanao toa maelekezo ni msaada mkubwa kwao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: