Katika mkutano na waandishi wa habari, Atabatu Abbasiyya tukufu yaeleza huduma ilizo toa kwa mazuwaru…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu leo Alkhamisi (19 Safar 1439h) sawa na (9 Novemba 2017m) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuelezea huduma za kiusalama na kimahitaji walizo toa katika kipindi hiki cha ziara ya Arubaini na kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu sekta hiyo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya vinavyo shiriki katika program za ziara ya Arubaini, ambavyo vimefanya na bado vinaendelea kufanya juhudi kubwa ya kuhakikisha mahitaji yote muhimu yanapatikana kwa watu walio kuja kufanya ziara ya Arubaini.

Mkutano huo ulihudhuriwa na naibu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na jopo la viongozi wa Ataba pamoja na maraisi wa vitengo pamoja na idadi kubwa ya waandishi wa habari wanao rusha matukio ya ziara ya Arubaini, na walijibu maswali ya waandishi wa habari na wakatoa ufafanuzi katika mambo yaliyo hitaji ufafanuzi na kila kitengo kikataja utendaji wake.

Katika kikao hiki ilielezewa mikakati kwa ujumla ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika ziara hii na ile iliyo tekelezwa, wakafafanua tofauti ya ziara hii na zilizo tangulia, pamoja na kusikiliza maswali na maoni kutoka kwa wana habari.

Naibu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Bashiri Muhammad Jaasim amesema kua: “Kwa mara ya kwanza katika ziara ya Arubaini tunafanya kikoa na vyombo vya habari kutokana na juhudi tukufu za kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kilicho waita waandishi wa habari, na wale walio itikia wito Mwenyezi Mungu awalipe kila la kheri, lengo lilikua ni kuuonyesha ulimwengu nafasi ya Ataba katika ziara hii, yameulizwa maswali kwa viongozi wa vitengo na wao wameyajibu, kila mmoja amejibu kulingana na kitengo chake, vyombo vya habari vimefanya juhudi kubwa ya kuujulisha ulimwengu kua Atabatu Abbasiyya inatoa huduma fulani kwa mazuwaru watukufu katika siku hizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: