Ni Karbala… Picha zilizo pigwa kutoka juu leo (19 Safar 1439h)…

Maoni katika picha
Roho zenye machungu, hazilazimishwi na yeyote, haziliwazwi na yeyote, zinalia kwa mapenzi, zinaumizwa na kutengana, na ndani yake moto wa mapenzi unawaka, picha yako ewe uliye chinjwa, imekaa akilini milele, wanapo uliza nani anastahiki kuliliwa huku, tunasema kwa fahari, ni wewe tu peke yako ewe baba wa watu huru, hii ni ahadi.

Kamera ya mtandao wa kimataifa Alkafeel ilifuatana na majemedari wa jeshi la anga la Iraq, wanao simamia ulinzi wa anga kwa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi na wanao shiriki katika kuimarisha ulinzi kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu (1439h), picha hizi zinaonyesha namna watu walivyo furika katika barabara zinazo ingia kwenye mji wa Karbala na katika sehemu ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya).

Mwenyezi Mungu akuze malipo yao na awajalie maombolezo mema na awape malipo mema…
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: