Kitengo cha habari kupitia maukibu ya wapenzi wa Alkafeel kinatoa huduma kwa mazuwaru…

Maoni katika picha
Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu hakija ishia kurusha habari na harakati za kitamaduni katika ziara ya Arubaini peke yake, bali wamekua na nafasi kubwa ya kutoa huduma zingine kwa mazuwaru kupitia maukibu ya wapenzi wa Alkafeel, maukibu hii tangu ianzishwe ina miaka mitatu, inatoa huduma kubwa kutokana na mahala ilipo, ipo katika panda njia muhimu ya kuelekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sehemu ambayo inamsongamano mkubwa wa watu, wahudumu wa maukibu hiyo wanajitahidi kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu.

Maukibu inaongozwa na watumishi wa kitengo hicho, miongoni mwao; wafanya kazi wa Maahadi ya Alkafeel ya elimu na kukuza vipaji, pamoja na wafanyakazi wa idara ya picha za video, na sehemu kubwa ya wafanyakazi wa idara na vitengo vingine pia, wanafanya kazi kama nyuki bila kuchoka wala kulegea katika kuhudumia mazuwaru watukufu.

Maukibu inatoa huduma mbalimbali na chakula na vinywaji, wanaanza kazi mapema asubuhi kwa kugawa chai (chakula cha asubuhi) na wanamaliza kwa kugawa chakula cha usiku baada ya kugawa chakula cha mchana, pia kuna vyakula vidogo vidogo ambavyo wanagawa siku nzima, havina muda maalumu, kama vile chai, maji, matunda na vinginevyo, wanufaika wa huduma hii kwa siku ni zaidi ya watu (8000) na baadhi ya mida hua kubwa zaidi.

Kumbuka kua maukibu hii huendelea kutoa huduma kwa mazuwaru wanao rudi makwao baada ya kumaliza ziara kwa ufanisi uleule, kwa kua maukibu nyingi hufunga kazi zao mara tu baada ya kumaliza ziara, hii ni miongoni mwa mawakibu za Atabatu Abbasiyya tukufu zilizo sajiliwa rasmi na kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: