Maukibu ya shamba boy wa Alkafeel ni moja ya anuani za ukarimu wa mwenye utukufu…

Maoni katika picha
Baada ya kufaulu kwake katika kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika miaka ya nyuma, bado maukibu ya kutoa huduma ya shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa huduma kwa mazuwaru, na wanafanya kazi kwa uwezo wao wote wa mali na watu.

Maukibu ipo katika moja ya barabara ndogo zinazo elekea Karbala, ambayo ni barabara ya (Husseiniyya – Karbala) imekua ni kituo cha mazuwaru wengi.

Maukibu inatoa milo mitatu mikuu, chakula cha asubuhi, mchana na jioni, inasifika kwa kupika chakula kizuri, na milo yake miwili (wa mchana na jioni) huandaliwa na nyama za kuchoma na samaki kutoka katika mabwawa yao, idadi ya wanufaika kwa kila siku inakaribia watu (3000) na huzidi hapo baadhi ya nyakati.

Pamoja na huduma hizo pia maukibu imeandaa kumbi tatu za kulala mazuwaru, moja ya wanaume na mbili za wanawake, pamoja na ukumbi wa kuswalia na sehemu za vyoo, maukibu hii huanza kazi mapema asubuhi na hufunga usiku mwingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: