Kikosi cha uokoaji cha Atabatu Abbasiyya tukufu chaokoa zaidi ya maafa elfu sita (6)…

Maoni katika picha
Kikosi cha uokoaji wa mazuwaru kimefanikiwa kuokoa zaidi ya maafa elfu sita (6000) ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu iliweka zaidi ya waokozi (350) ndani ya ukumbi wa haram tukufu, walio simama pembezoni mwa haram huku wengine wakisimama milangoni, kulikua na vituo vitano vya kutoa huduma za uokozi ndani ya ukumbi huo mtukufu.

Kiongozi wa kikosi cha madaktari walio endesha zoezi hilo Ustadh Bilali Jabaar Khafaji amebainisha kua: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeweka utaratibu wa kuokoa mazuwaru, hii ni kutokana na msongamano mkubwa wakati wa ziara, tumesambaza zaidi wa waokozi (350), na tumeweka vituo vitano vya kutolea huduma ndani ya ukumbi wa haram tukufu, viwili vya wanaume na vitatu vya wanawake”.

Akaongeza kusema kua: “Katika zoezi hili wameshiriki jumla ya madaktari (35) walio bobea katika fani mbalimbali, wanaume (15) na wanawake (20) pamoja na madaktari wengine (9) kutoka Pakistani”.

Akabainisha kua: “Katika kila kituo cha kutoa huduma kuna idadi kadhaa ya wauguzi, wauguzi wote jumla wapo (70) na jopo la mafamasia, miongoni mwao kuna wenye shahada za kisekula, pia walipata mafunzo ya utoaji wa huduma ya kwanza pamoja na namna ya kumbeba mtu aliye patwa na maafa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: