Kitengo cha dini kinajibu maswali ya mazuwaru na kutoa nasaha za kidini na maelekezo…

Maoni katika picha
Mwezi wa Muharam na mwezi wa Safar ni miongoni mwa miezi ambayo huonekana harakati za kitengo cha dini, katika kipindi cha ziara ya Arubaini wamefanya mambo mengi, kimeandaa watumishi wake, mashekhe na masayyid na kikawaongezea wasomi wa kujitolea miongoni mwa wanafunzi wa hauza.

Kitengo hiki kimeshiriki katika mradi wa tablighi ambao huendeshwa na hauza ya Najafu, kupitia vituo vya tablighi ambavyo hujibu maswali yote ya mazuwaru, ya kifiqhi, kiaqida na mengineyo miongoni mwa mambo ya dini, jukumu lao lingine hua ni kuswalisha jamaa katika maeneo waliopo pamoja na kutoa mihadhara ya kidini.

Hali kadhalika kitengo cha dini kina jukumu la kuchapa na kugawa maelfu ya machapisho mbalimbali kuhusu mafundisho ya dini, pamoja na mambo yanayo husu ziara na kutoa maelekezo kwa mazuwaru na kuwapa nakala za ziara ya Arubaini, kazi hizo hufanywa siku nzima.

Kwa upande mwingine kitengo cha dini kilikua na jukumu la kuendesha majalis ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kujibu maswali ya mazuwaru na kutolea ufafanuzi baadhi ya mambo ndani ya ukumbi au kwa kupitia mubalighina wake waliopo katika maeneo maalum ndani ya ukumbi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: