Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ashiriki katika maukibu ya kuomboleza: Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji chahuisha Arubaini…

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji mchana wa Ijumaa ya (20 Safar 1439h) kimeshiriki katika mkusanyiko wa mamilioni ya watu kwa kufanya matembezi ya maombolezo ya kuhuisha Arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Katika maukibu (matembezi) hayo walishiriki majemedari waliokua walinda amani na watoa huduma kwa mazuwaru, wakitanguliwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar na kiongozi mkuu wa kikosi hicho Shekh Maitham Zaidiy, pamoja na wabeba bendera na picha za baadhi ya mashahidi wa kikosi hicho.

Matembezi ya maombolezo yalianzia katika eneo la (Baabu tuwareji), huku wakiimba nyimbo za maombolezo na kuonyesha mapenzi yao kwa Imamu, wakatembea hadi katika kaburi la Imamu Hussein (a.s), kisha wakaingia katika ukumbi wa haramu yake (a.s) na wakatoka kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu wakaenda hadi katika malalo ya mbeba bendera ya Twafu Abulfadhil Abbasi (a.s), wakaingia katika ukumbi wa haram yake wakiwa wamejaa huzuni na majonzi makubwa, huku wanawakumbuka katika kila hatua ndugu zao vipenzi walio jitolea uhai wao kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matakatifu wakiwa wameshikamana na Hussein katika nyoyo zao.

Kisha wakafanya majlis ya maombolezo ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), halafu kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekh Maitham Zaidiy akatoa shukrani zake na pongezi kwa juhudi kubwa zilizo onyeshwa na askari wake wa kujitolea waliotoka mikoa mbalmbali ya Iraq na kuja Karbala kwa ajili ya kuimarisha usalama na kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu.

Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilicho kua na jukumu la kuhakikisha usalama wa mazuwaru katika ushiriki wake wa ulinzi, na chenyewe kimependa kutoa taazia katika tukio hili la kusikitisha kwa kufanya matembezi ya maombolezo ili kipate thawabu za ziara pamoja na mamilioni ya watu waliokuja kufanya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: