Kitengo cha utumishi chagawa maelfu ya blanket kila siku kwa mazuwaru…

Maoni katika picha
Siku za mwisho za ziara ya Arubaini zimeshuhudia kushuka kwa kiwango cha joto hasa katika nyakati za usiku mwingi, jambo lililo pelekea kua na baridi kali, ikalazimika kitengo cha utumishi kifungue hazina zake na kugawa mablanketi kiliyo kua kimeyaandaa kwa maelfu na kuyahifadhi katika maeneo ya karibu na wanapo lala mazuwaru watukuu.

Sehemu za kugawia mablanketi zinafunguliwa kila siku kuanzia saa tatu usiku na zinabaki wazi hadi asubuhi, kutokana na huduma hii wameweza kupunguza mateso ya baridi kwa mazuwaru na hasa kwa watoto na wazee, huku baadhi ya mablanketi yakitumika kama tandiko, pia tumetumia njia rahisi zaidi ya kutoa na kupakea mablanketi hayo.

Kumbuka kua kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo vinavyo toa huduma ya moja kwa moja kwa mazuwaru, na hufanya kila wawezalo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru waliopo ndani ya Ataba tukufu au katika maeneo ya nje, ndio maana kitengo hiki kiliongezewa watumishi wa kujitolea (2000) waliofanya kazi bega kwa bega na watumishi wa kitengo hicho katika kuhudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: