Kutokana na juhudi zao nzuri za kutangaza hali halisi iliyo kuwepo katika ziara ya Arubaini, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa shukrani za dhati kwa vyombo vyote vya habari vilivyo shiriki katika kutangaza matukio kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hayo yapo katika tamko rasmi lililotolewa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia katibu mkuu wake Muhandisi Muhammad Ashiqar: “Kwa vyombo vyote vya habari –Idumu taufiqi yenu- Tunatoa shukrani za dhati kwenu, kutokana na juhudi nzuri mliyo fanya katika kutangaza habari za maadhimisho ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ya mwaka 1439h, Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aiweke kazi yenu hiyo katika daftari la mema yenu, na akujalieni kupata kila kinacho mridhisha na kumfurahisha, hakika yeye ni msikivu wa maombi”.
Kumbuka kua ziara ya Arubaini ya mwaka huu ilikua na ushiriki mkubwa wa vyombo vya habari (Luninga –tv-, Redio na Magazeti) vya ndani na nje ya Iraq, wameweza kurusha picha halisi ya maadhimisho haya, taasisi na makampuni ya vyombo vya habari yalikua zaidi ya (250), pia kulikua na idadi kubwa ya wapiga picha wa kitaifa na kimataifa, idadi yao ilikua zaidi ya wapiga picha elfu kumi (10,000), wengi wao wanikua wanatokana na taasisi za vyombo vya habari tajwa hapo juu na mitandoa ya kielektrokik.