Baada ya kumaliza msimu wa Arubaini wa mwaka 1439h, na kuonekana mafanikio ya ulinzi wa usalama na kudumisha amani katika barabara kuu zote zinazo ingia Karbala, na kuwalinda mazuwaru, Wakili wa Marjaa dini mkuu Sayyid Ahmadi Swafi, amewapokea viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji pamoja na jopo la watendaji wake wa idara.
Sayyid Ahmadi Swafi amesifu “Juhudi za pekee zilizo fanywa na kikosi hicho pamoja na hali ngumu ya kifedha waliyo nayo”.
Sayyid Swafi ameonyesha shukrani zake za dhati, na akakiombea kikosi hocho kipate mafanikio na ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, kikosi hicho kilikua na jukumu kubwa la kulinda usalama wa mazuwaru, na kilitumia askari wake (3300) wakiwemo wapiganaji wazoefu na majemedari mahiri (1000).
Hali kadhalika kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesifu “Huduma zingine zilizo tolewa na kikosi hicho, kama vile huduma za afya, na utumiaji wa magari yake katika kubeba mazuwaru watukufu, na akasema kua walikua msaada mkubwa katika sekta zote za utumishi”.
Akaongeza kua: “Vile vile kikosi kilifanya jambo zuri kuweka hali ya tahadhari katika anga la Karbala, na kutoruhusu ndege kupita katika anga hilo kwa umbali wa kilometa 4 hadi kwa idhini ya Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) au uongozi wa jeshi la Karbala tukufu”.
Naye kiongozi mkuu wa kikosi hicho, Maitham Zaidiy akasema kua: “Hakika kikosi cha Abbasi (a.s) kilifanya kazi ya kuwakagua mazuwaru katika njia kuu zinazo ingia Karbala (barabara ya Najafu, Bagdad na Baabil), hakika kimefanya kazi kubwa ukilinganisha na kazi zilizo fanya na vikosi vingine vya Hashdi Sha’abi”.