Waziri mkuu wa Iraq: Miradi na huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu zinathaminiwa na serikali ya Iraq…

Maoni katika picha
Juma Mosi ya leo (21 Safar 1439h) sawa na (11 Novemba 2017m) waziri mkuu wa Iraq dokta Haidari Abadi amefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na baada ya kukamirisha ibada ya ziara akakutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la viongozi.

Waziri mkuu amesisitiza kupitia maandashi aliyo andika katika daftari la utawala kua:

Tumepata utukufu wa kutembelea kaburi la Abbasi bun Ali (a.s) na kukutana na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, huduma wanazo toa kwa mazuwaru watukufu kupitia miradi yao mikubwa ya kiutumishi na kiuchumi, sisi kama serikali tunazithamini sana, bila shaka zinathaminiwa na mazuwaru wote, Mwenyezi Munyu awawezeshe muendelee kufanya kheri zaidi.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi na rehema zake na baraka zake.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu imetekeleza mpango mkubwa wa kuwahudumia na kuwalinda mazuwaru watukufu waliokuja katika mji wa Karbala kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), idadi yao inakadiriwa kufika karibu watu milioni (14).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: