Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa maelezo kuhusu ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ya mwaka 1439 Hijiriyya…

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya siku ya Ijumaa (20 Safar 1439h) sawa na (10 Novemba 2017m) imetoa maelezo kuhusu idadi wa watu waliokuja Karbala kuhuisha ziara ya Arubaini.

Wametoa maelezo hayo katika tangazo la kukamilika kwa ziara ya Arubaini, na hii ndio nakala ya maelezo: “Amani iwe juu ya Hussein na Ali bun Hussein na watoto wa Hussein na maswahaba wa Hussein (a.s), tunatuma rambirambi kwa Imamu Hujjah (a.s) na Maraajii watukufu pamoja na ulimengu wa kiislamu kwa ujumla katika kukumbuka Arubaini ya Imamu Hussein (a.s). Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ailinde miji ya waislamu na kila baya, na awarejeshe mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) salama katika miji yao, na dua hii iwajumuishe ndugu zetu wapiganaji waliopo katika uwanja wa vita, nao pia waandikiwe thawabu za kufanya ziara, hakika ndugu zao hawakuwasahau katika dua zao.

Mji mtukufu wa Karbala umepata heshima ya kufikiwa na wageni wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), waliokuja kufanya ziara kwa mamilioni ya watu, watumishi wa Ataba tukufu ilikua heshima kubwa kwao kupata nafasi ya kuwakaribisha na kuwahudumia mazuwaru watukufu, walitoa huduma za aina nyingi, miongoni mwa huduma hizo ilikua ni kudhibiti idadi wa mazuwaru, ambayo ilifanywa kwa kufunga kamera maalumu za kuhesabu watu katika sehemu nne, barabara ya: (Bagdad – K arbala, Najafu – Karbala, Baabil – Karbala na Husseiniyya – Karbala), jumla ya idadi iliyo patikana kupitia sehemu hizo nne ni (13,874,818) kuanzia mwezi 7 – 20 Safar.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awakubaliye wote maombi yao, na atuwafikishe katika mambo anayo yapenda na kuyaridhia hakika yeye ni msikivu mwenye kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: