Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea mitambo ya matangazo ya moja kwa moja na asifu juhudi za watalamu wake katika ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi amesifu kazi nzuri iliyo fanywa na watalamu wa idara ya matangazo ya moja kwa moja iliyo chini ya kituo cha uzalishaji cha Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni, katika kurusha matangazo ya moja kwa moja kwenye ziara ya Arubaini.

Ameyasema hayo alipo tembelea mitambo ya matangazo ya moja kwa moja na kuongea na watalamu wake, matangazo yaliyo husisha sehemu mbalimbali, ikiwemo ya matembezi kuanzia mikoa ya kusini hadi Karbala, na sehemu nyingine ilikua ni ndani ya Ataba mbili tukufu, ambapo walirusha harakati zote za maombolezo bure bila kutumia masafa ya ndani, na matangazo yaliyo kua na picha nzuri kabisa.

Sayyid Ahmadi Swafi mwishoni mwa ziara yake, amewaomba watalamu wa idara ya matangazo ya moja kwa moja, waongeze juhudi zaidi, wasiishie hapo walipo, waitumie ziara hii kama msingi wa kujiandaa na ziara ijayo, akawahimiza wajitahidi kunufaika na maendeleo yaliyopo katika sekta ya utangazaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: