Mwezi ishirini na tatu Safar ni kumbukumbu ya kufariki kwa Fatuma bint Asad mzazi wa shujaa wa watoto wa Abu Twalib na mlezi wa Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo, mwezi ishirini na tatu Safar mwaka wa nne hijiriyya alifariki bibi mtukufu Fatuma bint Asadi (a.s), mke wa Abu Twalib na mzazi wa Imamu kiongozi wa waumini Ali (a.s), nanye ni mama mwenye heshima kubwa alikua katika dini ya nabii Ibrahim kabla ya kuja uislamu.

Inajulikana kwamba, pindi Abu Twalib alipo mletea Mtume (s.a.w.w) baada ya kufariki kwa Abdulmutwalib akamuambia: Tambua kua huyu ni mtoto wa ndugu yangu, nampenda kushinda nasfi yangu na mali zangu, ole wako yeyote amkere katika jambo analotaka, akatabasamu na akasema: Unanihusia kuhusu mwanangu Muhammad!!? Hakika mimi nampenda zaidi ya nafsi yangu na watoto wangu, Abu Twalib akafurahi kusikia hivyo.

Bibi Fatuma alionyesha mapenzi makubwa sana kwa Mtume (s.a.w.w), alikua akimpendelea zaidi kuliko watoto wake katika chakula na nguo, alikua anamuogesha na kumpaka mafuta na kutembea naye, na Mtume (s.a.w.w) pia alimpenda sana na alikua hamwiti kwa jina lingine zaidi ya mama.

Hakika bint Asadi ana nafasi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu, yeye ni katika waja wa karibu zaidi walio pata shifaa yake, pale alipo sema: (Wala uombezi mbele yake hauta faa kitu, isipo kuwa kwa aliye mpa idhini..), alipata nafasi hiyo akiwa hapa duniani, na kesho akhera atakua katika wale watakao ruhusiwa kuwaombea watu na Mwenyezi Mungu atakubali maombezi yake.

Hakupata nafasi hiyo isipo kuwa baada ya kumuamini Mtume (s.a.w.w) na kutakasika na ibada ya masanamu, na kudumu katika tauhidi, aliamini kua mtu dhaifu anaweza kufikia ukamilifu kwa kulinda nafsi yake kutokana na mabalaa na kushikamana na kumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja asiye kuwa na mshirika.

Miongoni mwa watakao salimika na moto wa Jahannamu ni Fatuma bint Asad, imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kuwa Mwenyezi Mungu alimpa wahyi Mtume wake (s.a.w.w): “Mimi nimeharamisha moto kwa mgongo ulio kutoa na tumbo lililo kubeba na miguu iliyo kulea na watu wa nyumbani kwako walio kusaidia”.

Abdullahi bun Abdulmutwalib ndio mgongo ulio mtoa, na tumbo lililo mbeba ni Amina bint Wahabi, na mikuu iliyo mlea ni Fatuma bint Asadi, na watu wa nyumbani kwake walio msaidia ni Abu Twalib.

Hakika Fatuma bint Asadi alionyesha mapenzi makubwa sana kwa Mtume (s.a.w.w) wakati wa udogo wake, na alimlea malezi ya mama kwa mwanaye kipenzi, Mwenyezi Mungu akamlipa kutokana na wema wake akamuharamishia moto.

Alifariki (a.s) katika mji wa Madina na Mtume (s.a.w.w) ndiye aliye simamia mazishi yake.

Siku moja Mtume (s.a.w.w) akiwa amekaa, aliijiwa na kiongozi wa waumini (a.s) akiwa analia, Mtume akamuulia: kitu gani kinakuliza? Akasema: Mama yangu Fatuma amefariki, Mtume akasema: Ni mama yangu pia, wakasimama na wakaenda haraka kumuangalia, Mtume akalia sana kisha akawaambia wanawake wamuoshe.

Mtume (s.a.w.w) akawaambia, mtakapo maliza kumuosha msifanye jambo lolote mnipe taarifa, walipo maliza kumuosha wakamjulisha, akawapa kanzu yake akawaambia wamvishe hiyo ndio sanda yake, akawaambia waislamu: Mtakapo niona nimefanya kitu ambacho sijawahi kufanya siku za nyuma niulizeni kwa nini nimefanya, walipo maliza kumvisha sanda Mtume (s.a.w.w) aliingia na akabeba jeneza mabegani kwake hadi kaburini, kisha akaingia kaburini na akamlaza katika kaburi lake, halafu akachukua muda mrefu akimuombea dua, na mwishoni akawa anasema: mwanao mwanao mwanao, halafu akatoka na wakamfunika kwa udongo, kisha akainama juu ya kaburi akasikika anasema: Hakuna Mola isopo kuwa Allah, Ewe Mola mimi namuacha kwako, kisha akaondoka.

Waislamu wakasema: Hakika tumekuona umefanya mambo ambayo haujawahi kuyafanya kabla ya leo. Akasema: Leo nimemkosa mtu mwema kwangu katika nyumba ya Abu Twalib, ikiwa kuna kitu (kibaya) kitafanyika kwake (kitaniumiza) mimi na mwanae, mimi nilimuelezea hali ya siku ya Kiyama, kua watu watafufuliwa bila nguo, akasema: Ole wangu kukaa bila nguo, nikamuahidi kua Allah atamfufua na nguo, nikamuambia kua kaburi hubana watu, akasema: Ole wangu mimi ni dhaifu, nikamuahidi kua kaburi halita mbana, ndio maana amevishwa kanzu yangu, na nimemuweka mwenyewe ndani ya kaburi na kumuambia mambo atakayo ulizwa (kumsomea talakini), akaulizwa kuhusu Mungu wake akajibu, na akaulizwa kuhusu mtume wake akajibu, akaulizwa kuhusu kiongozi wake na Imamu wake akababaika, ndipo nikamuambia, mwanao, mwanao, mwanao (Usulul Kaafi 1/515 h2).

Kaburi lake tukufu lipo katika makaburi ya Bakii karibu na makaburi ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), bibi mtukufu Fatuma bint Asad (a.s) kutokana na ikhlasi yake amekua ni walii miongoni mwa mawalii wa Mwenyezi Mungu ambao watu hufanya tawasul kwao katika kumuomba Mwenyezi Mungu awatatulie matatizo magumu yanayo wasibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: