Kwa picha: Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) bado unaendelea kuwapa chakula mazuwaru wa Arubaini…

Maoni katika picha
Pamoja na kupita siku nne tangu kumalizika kwa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), lakini mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) bado unaendelea kugawa chakula kwa mazuwaru waliofika kwa kuchelewa katika mji mtukufu wa Karbala au waliobakia na asilimia kubwa ni wale wanaotoka nje ya Iraq.

Watumishi wa mgahawa wanaendelea kutoa huduma ya chakula milo mitatu kwa mazuwaru bila kuchoka, na wanaendelea kugawa chakula katika vituo vya nje ya mgahawa kama ilivyo pangwa na wanajitahidi kumpa chakula kila anaye wafikia.

Kumbuka kua mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kipindi cha ziara ya Arubaini walitoa huduma ya chakula saa 24 kila siku, pia walikua wanapokea wageni na kuwaandalia chakula, kila siku waligawa zaidi ya sahani za chakula elfu (45) katika milo mikuu mitatu, ugawaji wa chakula ulifanyika ndani ya ukumbi wa mgahawa na katika madirisha sita ya nnje yaliyo andaliwa kwa shughuli hiyo.

Mazuwaru walisifu huduma hii tukufu, wakaichukulia kua ni miongoni mwa zawadi kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: