Wanadamu walijifakharisha kwa viumbe wengine wote kua Muhammad (s.a.w.w) anatokana na wao, na aridhi ikajifaharisha kwa mbingu kua Karbala inatokana nayo.
Kutokana na utukufu wa mji huo kila mtume na nabii alikusudia kuutembelea, nao ni mji wa Karbala, aridhi takatifu iliyo muhifadhi bwana wa mashahidi mjukuu wa Mtume Imamu Hussein (a.s), kwa kua mji huu ni mtukufu katika kila zama, wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wanafanya juhudi ya kutengeneza kopi ya mji huo katika kila sehemu ya dunia.
Majimbo mengi ndani ya Marekani, wapenzi wa Ahlulbait wamejitokeza na kufanya maadhimisho ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), wamefanya matembezi na kupandisha bendera ya Hussein (a.s) pamoja na mabango yaliyo andikwa ujumbe tofauti, yakiwemo yaliyo andikwa kuhusu msiba na mengine maswala ya haki za binadamu na kupinga ubaguzi, kwa sababu Hussein ni wawote, waislamu wanao ishi katika majimbo yaliyo fanya maadhimisho hayo walishiriki katika matembezi bamoja na wasio kua waislamu, kwa sababu Hussein ni baba wa watu huru duniani kote na katika kila zama.
Picha hizi ambazo zimepatikana kutoka katika vyanzo vya (mtandao wa kimataifa Alkafeel) zinaonyesha namna maukibu (kikundi) cha maomboleza na cha kutoa huduma walivyo fikisha ujumbe kwa walimwengu, hakika njia ya kuelekea Karbala ndio njia ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wa kila sehemu hapa duniani.