Kwa ajili ya kukumbuka kifo cha Mtume (s.a.w.w) Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa ratiba ya maombolezo…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuombeleza kufariki kwa Mtume (s.a.w.w) ambako kutasadifu siku ya kesho Juma Mosi 28 Safar 1439h, ratiba inayo endana na msiba huu mkubwa wa kuondokewa na Nabii wa rehema na muombezi wa Umma, aliye teuliwa katika binadamu kua muongoaji, mkumbushaji na nuru, alichaguliwa kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

Ratiba hiyo itapambwa na majlisi za maombolezo, matam na utoaji wa mihadhara ya kidini, itakayo elezea historia ya Mtume (s.a.w.w) na baadhi ya sifa zake pamoja na sehemu za wasia wake na mambo aliyo tilia msisitizo (s.a.w.w), kama vile kushikamana na uongozi wa Imamu Ali (a.s), pia yamewekwa mabango mengi yaliyo andikwa hadithi na usia wake (s.a.w.w) katika sehemu mbalimbali ndani ya ukumbi wa haramu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Pamoja na hivyo kesho siku ya Juma Mosi mchana watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) watafanya matembezi ya pamoja kwenda kumpa taazia Imamu Hussein (a.s) kutokana na msiba huu, matembezi hayo yatatanguliwa na majlisi ya kuomboleza itakayo fanyika katika ukumbi wa utawala ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Amma kuhusu upande wa utoaji wa huduma, Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa kupokea mazuwaru na mawakibu (vikundi) vya waombolezaji watakao kuja katika haramu hiyo tukufu, kutoka ndani na nje ya Karbala, pamoja na mazuwaru watakao toa taazia kwa Imamu Ali (a.s) kwa kuja katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua kifo cha mwisho wa Mitume na Manabii Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w) kilikua siku ya mwezi 28 Safar mwaka wa 11 Hijiyya, akiwa na umri wa miaka 63, waumini wengi katika mnasaba huu, hua wanakwenda katika kaburi la simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda Ali bun Abu Twalib (a.s), kwa ajili ya kufanya taazia na kuomboleza kumbukumbu ya msiba wa kipenzi chake na ndugu yake mtoto wa ammi yake Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w) nayo ni miongoni mwa ziara maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: