Kwa picha: Watu wa Karba watoa taazia kwa kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Jioni ya siku ya Ijumaa (27 Safar 1439h) sawa na (17 Novemba 2017m) maukibu ya watu wa Karbala ilielekea katika mji wa Najafu kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w), na kufanya maombolezo kwa ndugu yake, khalifa na wasii wake kiongozi wa waumini (a.s) na kuhuisha utiifu kwake na kukumbuka masomo na kupata mazingatio kutokana na mwenendo ya Mtume (s.a.w.w).

Wamefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram tukufu ya Alawiyya, majlis iliyo pambwa na kaswida zilizo elezea undani wa msiba huu, washiriki walikua wanasema maneno ya kuomboleza wakiwa na huzuni kubwa na kutuma pole zao kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), matembezi yao yalipambwa na kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni.

Kumbuka kua maukibu hii ya kuomboleza hufanywa kila mwaka na watu wa Karbala katika kuhuisha kumbukumbu za minasaba mbalimbali za Ahlulbait (a.s), inaundwa na mawakibu tofauti pamoja na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala pamoja na kundi la wakazi wa mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: