Kwa picha: Makundi ya watu wanahuisha kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w) katika malalo ya mtoto wa ammi yake na wasii wake (a.s)…

Maoni katika picha
Mamilioni ya watu kutoka ndani na nje ya Iraq wamehuisha kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w) katika malalo ya mtoto wa ammi yake na wasii wake Ali bun Abu Twalib (a.s), kwa ajili ya kumpa pole kutokana na msiba huu, chini ya ulinzi mkali na huduma bora zinazo tolewa na Atabatu Alawiyya tukufu pamoja na sekta zingine za ulinzi na utumishi.

Makundi makubwa ya watu wamekuja kutoka katika mikoa tofauti na wengi wao wametembea kwa miguu, wakiwa na nia ya kuhuisha tukio hili la majonzi, huku wengi wao wakitembea zaidi ya siku tatu, maukibu za kutoa huduma jimejaa katika barabara zote zinazo elekea katika mji mtukufu wa Njafu, pamoja na kuwepo kwa majengo ya malazi ya karibu, wananchi wa Iraq wameshiriki katika maombolezo haya pamoja na ndugu zao kutoka nje ya nchi walio kuja katika ziara ya Arubaini na ambao bado hawajaondoka hadi sasa.

Kumbuka kua miongoni mwa mambo bora yaliyo himizwa katika riwaya za watu wa nyumba takasifu ya Mtume (a.s) ni kumzuru kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu hii ya majonzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: