Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanasema: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe Abu Abdillahi…

Maoni katika picha
Katika kukumbuka kifo chako ewe uliye tumwa kuwa rehma kwa walimwengu tuna maumivu yasiyo fananishwa na chochote mbinguni wala aridhini, kwetu ulikua sawa na upepo, ulipo fikwa na kifo upepo haukuweza kufanya kazi, wewe ndiye mbeleko (bebeo) la zama, kutokana na wewe tumeamini tukapata bishara njema na tukapata uombezi mbele ya Mwenyezi Mungu, Labbaika alfu labbaika ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Wito unaotolewa na nyoyo za watumishi wa Atabatu Abbasiyya katika kila hatua wanayo piga, huku wakitoa taazia kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib na kwa Hassan na Hussein na kwa Imamu wa Zama (a.s).

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walifanya matembezi ya maombolezo kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) kumpa pole kutokana na msiba huu mkubwa unao waumiza Ahlulbait na umma wa kiislamu ulio tokea siku kama ya leo, wakipitia katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku wakiimba kaswida za kuomboleza wakiwa wamejaa huzuni kwa kuondokewa na Mtume mtukufu (s.a.w.w).

Matembezi hayo yaliongozwa na kiongozi wa Ataba tukufu pamoja na watumishi, wakaingia katika ukumbi mtukufu wa haram ya Imamu Hussein, na wakashirikiana na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na viongozi wa vitengo vyake kufanya majlis ya kuomboleza msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: