Wanafunzi na walimu wa shule ya Al-Ameed na Saaqi wafanya kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w) katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Bado zinaendelea mawakibu za kuomboleza ambazo hufanywa kila mwaka na shule za Abulfadhil Abbasi (a.s), zilizo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Abatatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya leo (19/11/2017m) shule mbili za (Al-Ameed na Saaqi), wanafunzi wa elimu ya msingi katika shule hizo wamefanya matembezi ya kuomboleza na kumpa pole Imamu wa zama (a.f) katika kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume wa ubinadamu na rehma Muhammad (s.a.w.w).

Kitendo hiki kinachukuliwa kua ni moja katika masomo ya nje ya darasa yanayo lenga kujenga uwelewa wa wanafunzi kuhusu mwenendo wa Mtume mtukufu (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), na kinasaidia kuwakuza kijamii na ki-itikadi, na kuwafanya wafungamane vilivyo na imani yao sahihi.

Matembezi hayo yalihusisha wanafunzi (600) pamoja na walimu wao, na yalihudhuriwa na kiongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambaye amesifu hatua hiyo na akasema ni sehemu muhimu ya malezi kwa watoto, inawafanya wawe na tabia nzuri na wafuate mwenendo mwema aliokuja nao Mtume Muhammad (s.a.w.w), na akawapa pongezi kubwa walio andaa jambo hili jema katika malezi ya kiislamu.

Hali kadhalika matembezi hayo yalipambwa na kaswida zilizo onyesha mapenzi makubwa kwa Mtume mtukufu na watu wa nyumbani kwake (a.s) kutoka kwa wanafunzi, kisha walifanya majlis ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi.

Tambua kua wanafunzi wa shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) wa ngazi zote, hufanya maombolezo kama haya kila mwaka, na huanza na wanafunzi wa ngazi ya chini
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: