Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya makhatibu wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua milango ya usajili kwa wanaotaka kujiunga nayo…

Maoni katika picha
Baada ya kupatikana mafanikio katika Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) chini ya idara ya makhatibu (wahadhiri) wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao wanatumia ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama makao makuu yao, wameandaa mimbari maalumu inayo tumiwa na wahadhiri wa kike wenye elimu nzuri kufikisha ujumbe kwa kufuata vigezo na kanuni za kielimu sambamba na maendelea ya leo.

Maahadi imefungua milango ya usajili kwa wanawake wanaopenda kujiunga nayo ili wawe watumishi wa mimbari ya bwana wa mashahidi (a.s), na wanafuata taratibu za ufundishaji unao tumiwa na taasisi (shule) zingine, masomo yatakayo fundishwa ni:

  • 1- Usomaji sahihi wa Qur’an tukufu.
  • 2-
  • 3-
  • 4-
  • 5- Tafsiri ya Qur’an.
  • 6- Manaahiju Bahthi (taratibu za utafiti).
  • 7- Utoaji wa khutuba (muhadhara).
  • 8-
  • 9-
  • 10- Maendeleo ya binadamu.

Kutakua na mazoezi ya kutoa mihadhara kwa kufuata kanuni na taratibu zilizo fundishwa. Fahamu kua muda wa masomo ni miaka mitatu, kisha wahitimu watapewa vyeti na Maahadi.

Usajili unaendelea katika makao makuu ya Maahadi ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu kwa namba zifuatazo: (07810645244 au 07602334055).

Lengo kuu la kuanzishwa kwa Maahadi hii ni kuongeza idadi ya mubalighina wa kike, kutokana na umuhimu wao hususan katika kipindi cha matukio ya maombolezo, na kuwafanya wawe na ushiriki mkubwa katika kuelezea muhanga wa Imamu Hussein (a.s), tena wauelezee kwa ustadi na weledi wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: