Miongoni mwa ushujaa wa Imamu Ali (a.s) ni kulala kwake kwenye kitanda cha Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Mwezi wa Rabiul-Awwal una mambo mengi ya kihistoria yaliyo tokea katika umma wa kiislamu, miongoni mwa matukio hayo ni kulala kwa Imamu Ali (a.s) katika kitanda cha Mtume (s.a.w.w), katika usiku wa kwanza wa mwezi huu mwaka wa (13) wa utume, tendo hilo linaonyesha ujasiri aliokua nao kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Historia haijaripoti kisa kingine kinacho onyesha kujitolea kwa hali ya juu kama huku, viongozi wa makuraishi walikubaliana kumuua Mtume akiwa katika kitanda chake, Mtume (s.a.w.w) akatambua njama hiyo na akamuambia Ali, Akalia kwa kuhofia usalama wa Mtume, lakini baada ya Mtume kumuambia alale katika kitanda chake, Ali akasema: Nikikulinda kwa nafsi yangu (nikilala kitandani kwako) utasalimika ewe mtume wa Mwenyezi Mungu? Mtume akasema: Ndio, hivyo ndio alivyo niahidi Mola wangu. Ali akatabasamu na kufurahi sana baada ya kujua kua Mtume atakua salama, akalala katika kitanda cha Mtume na akajifunika shuka yake akiwa na furaha na roho tulivu kabisa.

Ali (a.s) alilala katika kitanda cha Mtume (s.a.w.w) akiwa anajua wazi kua atauliwa, vijana wa makuraishi wakaja kutekeleza azma yao, walipo taka kumkatakata mapanga huku wakijua wazi kua aliye lala pale ni Mtume Muhammad (s.a.w.w), ghafla wakaona uso wa Ali (a.s), wakatoka ndani na kumuacha, halafu wakatawanyika kwenda kumtafuta Mtume (s.a.w.w).

Kabla ya kuhama kwa Mtume (s.a.w.w) alienda kwa Ali (a.s) akamuambia aende katikati ya mji wa Maka na awatangazie watu yeyote aliye kua na amana yake kwa Muhammad aje tumrejeshee, kisha Mtume akamuambia: watu watakujia na uwarejeshee amana zao nilizo kua nazo mbele ya macho ya watu (kwa wazi).

Mtume (s.a.w.w) alipo fika katika mji wa Madina akamuandikia Ali bun Abu Twalib (a.s) barua ya kumtaka amfuate Madina.

Imamu Ali (a.s) akaondoka Maka na kuelekea Madina akiwa na Fatuma bint Rasulu Llah (s.a.w.w), na mama yake Fatuma bint Asadi na Fatuma bint Zuberi bun Abdulmutwalib, akakutana na kundi la Makuraishi, akawaambia: mimi naenda kwa mtoto wa Ammi yangu, anayetaka kumwaga damu yake anifuate au asogee karibu yangu, kisha Imamu Ali akaendelea na safari yake pamoja na wakina Fatuma huku wanamtaja Mwenyezi Mungu mtukufu katika hali zote, wakiwa wamesimama au wamekaa.

Walipo fika Madina, ikateremka aya ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Mola mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanaume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi..) Al-Imraan: 195. Mtume (s.a.w.w) akawasomea aya hiyo, akasema wanaokusudiwa katika aya hiyo ni Ali (a.s) na wanawake walio safari nao (wakina Fatuma), kisha akamuambia Ali: (Ewe Ali! Wewe ni mtu wa kwanza katika umma huu kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wewe ni wakwanza kuhamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ni wamwisho utakaye kua pamoja na Mtume wake, –Namuapia yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake- Hatakupenda ispokua mu-umin, yule ambaye Mwenyezi Mungu amejaza imani katika moyo wake, na hatakuchukia ispokua mnafiki au kafiri).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: