Atabatu Abbasiyya tukufu imeratibu kongamano la Mtume mtukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Basra…

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa miradi ya kijana wa Alkafeel mzalendo. wameandaa kongamano liitwalo: (Kongamano la Mtume mtukufu la kitamaduni) linalo fanyika asubuhi ya Juma Tatu (1 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (20 Novemba 2017m) kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Basra. Hili ni kongamano la kwanza linalo fanywa kwa ajili ya kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume (a.s.w.w) na ni sehemu ya muendelezo wa makongamano mengi yanayo fanywa na vyuo mbalimbali vya Iraq.

Hafla ya kongamano hili imefunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba, kisha ukafuata ujumbe wa mkuu wa kitivo cha Sayansi dokta Falhi Abdul-Hassan Ali, ambaye alisema kua: “Tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuendesha makongamano kama haya ya kuadhimisha matukio muhimu na yenye athari kubwa kwa waumini, likiwemo kongamano hili la kukumbuka kufariki kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), walimu na wanafunzi wa chuo chetu wapo mstari wa mbele katika kufanya na kushiriki katika makongamano ya kitamaduni na kidini, ulikua utukufu mkubwa sana kwetu kupata nafasi ya kushiriki katika kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini katika Ataba tukufu, pia ilikua heshima kushiriki katika maukibu ya vyuo vikuu vya Iraq na kutoa heshma kwa baba wa watu huru -Abul-Ahraar- (a.s).

Akaongeza kusema kua: “Leo tunashiriki pamoja na umma wa kiislamu kukumbuka kufariki kwa Mtume (s.a.w.w), na kongamano hili ni moja ya njia za kuhuisha msiba huu mkubwa, na limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi ambao pia hawakubaki nyuma katika kuitikia mwito wa Marjaa dini mkuu ambaye ni kielelezo cha kuendelea kwa ujumbe wa Mtume, na kusimama pamoja na raia wa Iraq na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na kila mtu anaye pambana na magaidi wa Daesh, jambo ambalo limesaidia kupatikana ushindi kwa utukufu wa damu za mashahidi na kujitolea kwao kwa ajili ya kulinda na kuhami aridhi hii tukufu”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na naibu katibu mkuu Muhandisi Bashiri Muhammad Jaasim Rabii, ambaye amesema kua: “Ni fursa nzuri kwetu kukutana na walimu pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu cha Basra katika kumbukumbu ya kufariki kwa mtume mtukufu, ili tuweze kujifunza kwa pamoja kutoka kwa Mtume, umuhimu wa kusoma na kuitumikia jamii, natoa wito kwa wanafunzi watukufu mpambike na tabia za Mtume (Amekua kwenu Mtume ni kiigizo chema), ni matarajio yangu watu wote walio shiriki katika kongamano hili, wafuate nyayo za mtume na watu wa nyumbani kwake, na washikamane nao viliyo na kuwafanya kua taa lao”.

Kongamano likaendelea na ratiba ya mashairi kutoka kwa washairi mahiri yaliyo onyesha mapenzi ya dhati kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na kuwasifu na kuwatakia rehema mashahidi watukufu wa Iraq.

Kisha wakapeana zawadi wajumbe wote wa Ataba na wale waliotoka chuo kikuu cha Basra, na zikatolewa zawadi kwa kamati ya maandalizi ya kongamano hili, halafu yakafunguliwa maonyesho ya kikosi cha Abbasi (a.s), ambapo walionyesha picha za mashahidi wa kikosi hicho pamoja na baadhi ya ngawira walizo teka kudoka kwa magaidi ya Daesh katika vita, pia kulikua na maonyesho ya picha za kituo cha turathi za Karbala na maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel ya vifaa kale na nakala kale.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: