Baada ya kumaliza msimu wa huzuni za familia ya Muhammad (a.s): Vazi linalo ashiria huzuni na alama nyeusi zimeondolewa katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Baada ya kutangazwa kuandama kwa mwezi wa Rabiul-Awwal, watumishi wa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya wameanza kazi ya kuondoa vitambaa vinavyo ashiria huzuni vilivyo kua vimewekwa kila sehemu ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kipindi cha miezi miwili, mwezi wa Muharam na Safar, na wametangaza kumalizika kwa kipindi cha huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kuupokea mwezi wa Rabiul-Awwal.

Kazi hiyo imefanywa kwa hatua, hatua ya kwanza wamebadilisha bendera nyeusi iliyo kuwepo juu ya kubba tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka bendera nyekundu, na kazi hiyo ilifanya na masayyid, kisha wakahamia katika korido za haram tukufu, na walianza na kuondoa vitambaa vyeusi vilivyo kuwepo katika dirisha ya kaburi tukufu, na baada ya hapo wakaenda kuondoa kitambaa cheusi kilicho kua kimefunika ukuta wa haram tukufu ndani na nje, halafu wakazima taa nyekundu na kuwasha taa za kijani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: