Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chaweka aplikesheni (App) yake katika simu za kisasa (smartphone)…

Maoni katika picha
Watalamu wa idara ya Intanet kwenye kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanikiwa kutengeneza aprikesheni (App) ya simu za kisasa (Smartphone), aprikesheni (App) hiyo itahusika na iOS katika hatua ya kwanza na itaonyesha harakati zote zinazo fanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chini ya Ataba tukufu.

Aprikesheni hiyo itamsaidia mtumiaji kuangalia habari ya mwisho na harakati zinazo fanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, na itakua kiunganishi kati ya kitengo na wafuatiliaji wake, pamoja na kuwepo kwa toghuti yake rasmi, yanafanywa haya chini ya sera ya kunufaika na maendeleo mapya ya kisasa.

Aprikesheni (App) hiyo inamilango (kurasa) nyingi, miongoni mwake ni: Habari, Machapisho yake, Habari za vituo vilivyo chini yake na harakati zao pamoja na ukurasa wa picha na sauti.

Namna ya kupakua aprikesheni (App) hii bonyeza:

https://play.google.com/store/apps/details?id=iq.mk.almaaref

Kumbuka kua kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu ni moja ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimejikita katika sekta ya elimu na maswala ya kitamaduni kwa jamii nzima, na kusambaza fikra za Ahlulbait (a.s) kupitia idara zake na vituo vyake mbalimbali, kama vile: Maahadi ya Qur’an tukufu kwa wanaume na wanawake, kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla, kituo cha turathi za Basra, shule za Alkafeel za dini upande wa wasichana, idara ya habari, kitengo hiki kinalenga kutengeneza jamii bora kupitia harakati zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: