Miongoni mwa ratiba ya kongamano la Mtume mtukufu ni: Hafla ya usomaji wa Qur’an na utoaji wa muhadhara..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya kongamano la Mtume mtukufu la kitamaduni linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ambalo ni sehemu ya miradi ya kijana wa Alkafeel kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Basra mchepuo wa sayansi, jioni ya jana Juma Tatu (1 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (20/11/2017m), ni muhadhara wa mafundisho ya dini uliotolewa na Shekh Dakhil Nuriy kutoka katika kitengo cha dini cha Ataba tukufu, alio utolea katika sehemu ya kuswalia ya chuo na kuhudhuriwa na wanafunzi wengi.

Katika muhadhara wake alielezea umuhimu wa kupambika na tabia njema alizo himiza Mtume wa rehma na ubinadamu Muhammad (s.a.w.w), kwani elimu kubwa isiyokua na tabia njema haina faida, tabia njema na elimu kila kimoja kinamtegemea mwenzake, hali kadhalika akasisitiza kufuata mwenendo wake na wa watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s), na kuhakikisha tunaishi kwa kufuata mwenendo huo tuwapo chuoni, nyumbani na barabarani, pia wanafunzi walio hudhuria majlis hiyo waliuliza maswali mbalimbali ya kifiqhi na kiaqida kwa Shekh, naye alijibu maswali yao.

Kabla ya muhadha huo jopo la wanafunzi na wasomi wa Ataba tukufu walisoma Qur’an tukufu, na wakamalizia tena kwa visomo mbalimbali vya Qur’an tukufu, kisha wakasoma mashairi ya huzuni kufuatia kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: