Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi chakamilisha maandalizi ya vita ya kukomboa kisiwa kikubwa (kubra) na chawaahidi Daesh ushujaa wa wairaq unaotokana na Abbasi utawamaliza…

Maoni katika picha
Baada ya vikosi (bruged) zote za wapiganaji wa Abbasi (a.s) kukamilisha maandalizi yao, na kujikusanya kusini mwa Mosul kwa ajili ya kusubi amri ya kuanza kwa vita ya mwisho, makamanda wa Alkafeel wametangaza kua wako tayali kwa vita waliyo lazimishwa na adui wao na wamekua wakipigana kwa miaka mitatu na zaidi sasa, wanasubiri kugonga saa ya kuanza kwa vita hiyo kwa hamu kubwa, nayo inatarajiwa kua vita ya kusafisha maeneo ya mwisho kabisa yanayo kaliwa na magaidi wa Daesh katika aridhi ya Iraq, aridhi ya mitume na waja wema, makazi ya wasomi na maimamu watakasifu.

Mkuu wa kikosi Shekh Maitham Zaidiy ametangaza kua: “Hakika kikosi cha Abbasi (a.s) wataingia upande wa jangwa kwa kupitia kusini mwa mji wa Mosul sehemu ambayo ni muhimu sana katika vita hii, na watasonga mbele hadi wakutane na vikosi vya jeshi vitakavyo ingilia upande wa kaskazini ya mji wa Ambaar katika sehemu ya kwanza ya vita hii, na wamemuahidi adui kua ataona ushujaa na ujasiri wa wairaq unao tokana na kamanda aliye ongoza jeshi la haki kabla ya miaka 1378h Abulfadhil Abbasi (a.s) katika aridhi ya Karbala dhidi ya Madaesh wa zama zake.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kikosi kinakusudia kumaliza kabisa uwepo wa Madaesh katika aridhi ya Iraq na kulinda mipaka ili isitokee kuingia kwa hatari na ufunjifu wa amani”.

Kumbuka kua kikosi kimekamilisha maandalizi yote ya vita ya kukomboa kisiwa kikubwa kinacho unganisha baina ya mji wa Mosul, Swalahu-Dini na Ambaar, na watahakikisha wana wasafisha kabisa Madaesh walio kimbilia katika kisiwa hicho kutoka katika maeneo mbalimbali kwenye viwanja vya vita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: