Kwa kushiriki watu wa kujitolea kutoka katika vikundi vya Husseiniyya, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaendelea kufanya usafi katika mji wa Karbala…

Maoni katika picha
Miongoni mwa kazi zinazo fanywa na vitengo vya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya Juma Tano ya leo (3 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (22 Novemba 2017m), watumishi wa kitengo cha utumishi na wale wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, wameendelea na kazi ya kufanya usafi katika mji wa Karbala, kazi ambayo waliianza tangu kumalizika kwa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Kazi hii inafaywa kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, vitengo vinavyo wajibika na jukumu usafi vilianza kazi ya kusafisha barabara kuu ya (Karbala – Najafu), mapema leo asubuhi, baada ya kumaliza kusafisha eleo la mji wa zamani na barabara zake hapo awali.

Rais wa kitengo cha utumishi bwana Khalil Hanun ambaye anasimamia yeye mwenyewe kazi hii, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hii ni sehemu ya kukamilisha kazi iliyo anza kufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusafisha mji wa Karbala baada ya kumaliza ziara ya Arubaini, tulianzia kusafisha mji wa zamani wa Karbala na tutamalizia katika mji wa Khani Nasu uliopo katikati ya Najafu na Karbala, kazi hii imefanyika kwa siku kadhaa sasa, inafanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakishirikiana na watu wa kujitolea bamoja na magari ya usafi”.

Akaongeza kusema kuhusu umuhimu na malengo ya usafi huu: “Lengo la kazi hii ni kuuweka mji wa Karbala katika muonekano mzuri na kuondoa uchafu katika barabara ndogo na kubwa zote, tunatarajia kukamilisha kazi hii mapema iwezekanavyo”.

Tunapenda kukumbusha kua Atabatu Abbasiyya tukufu; baada ya kumaliza ziara ya Arubaini walianza mara moja kazi ya kusafisha maeneo yote ya mji mtukufu wa Karbala, kwa kushirikiana na vikundi vya Husseiniyya vilivyo shiriki katika ziara ya Arubaini, pamoja na kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu na kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: