Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amesisitiza kua turathi ni alama muhimu ya ubinadamu na zina umihimu mkubwa katika kuendeleza uhai wa umma, pia zina nafasi kubwa ya kujenga umoja na mshikamano katika jamii.
Ameyasema hayo katika kikao cha nadwa kilicho endeshwa na kituo cha turathi za Barsa chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kilicho fanyika asubuhi ya Alkhamisi ya leo (4 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (23 Novemba 2017m) kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dhiqaar/ mchepuo wa malezi na sayansi ya mwanadamu, nadwa iliyo kua na kauli mbiu isemayo (Basra baina ya turathi za kale na fikra mpya).
Ambapo alisema kua: “Turathi ni alama za ubinadamu, zina umuhimu mkubwa katika kuendeleza uhai wa umma na mataifa, zina nafasi kubwa ya kujenga umoja na mshikamano katika jamii, nazo ni kaika mambo ambayo binadamu hutilia umuhimu kuyasoma, ili anufaike na uzoefu wa watu walio tangulia, kwa hakika watafiti wamekua wakifanya hivyo toka zamani katika uandishi wa historia, kutokana na faida nyingi za kufanya hivyo, hakika kusoma historia za watu wa zamani na athari zao kuna tusaidia kujiepusha na makossa kama waliyo fanya wao”.
Akaongeza kusema kua: “Kila mtu anajua umuhimu mkubwa wa turathi, ni moja ya nyenzo muhimu katika kuweka mustaqbali wa mji, Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua chukumu la kuhuisha na kuzienzi turathi katika miji mbalimbali na kuanzisha vituo vya turathi katika miji hiyo, na tulianza na mikoa ya (Karbala – Hilla na Basra) mikoa hiyo ina historia na tamaduni za pekee, na kuifanya kua sawa na taa liwakalo katika zama hizi, kwa mfano Basra ni mkoa wenye tamaduni na historia kubwa, mkoa huo ulitoa wasomi wakubwa wa fani mbalimbali”.
Akasema kua: “Lengo la kufanya nadwa kama hizi ni kujaribu kukusanya turathi za mji wa Basra, na kuweka wazi mchango wa wasomi (wanachuoni) wao katika maswala ya kielimu, kiutafiti na kitamaduni, na kuwaunganisha watafiti pamoja na kusaidia mwenendo wa elimu katika sekta ya turathi za kifikra”.