Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kua wapiganaji wake wamemaliza siku ya kwanza katika vita ya kukomboa kisiwa kikubwa na wamefanikiwa kukomboa eneo la kilometa 45 na kudhibiti uwanja wa ndege wa jiniva kusini ya mji wa Hadhar katika mkoa wa Mosul sasa ndege zitaweza kutua na kuruka katika uwanja huo.
Wakaongeza kusema kua; kikosi cha wahandisi nacho kimefanikiwa kutegua mabomu ya kutega aridhini na kusafisha kabisa makumi ya kilometa za barabara zinazo tumiwa na wapiganaji hao.
Kumbuka kua maeneo yaliyo kombolewa ni ya vijiji vya (Burait, Samnu, Shaikhaan na Shaikha) na wanadhibiti kituo kikuu cha mawasiliano pamoja na magari ya magaidi ya Daesh waliyo yaacha na kukimbia.
Kumbuka kua viongozi wa kijeshi wanao ongoza opresheni hii wametangaza Alkhamisi ya leo (23 Novemba 2017m) kuingia hatua ya pili ya vita ya kukomboa maeneo yanayo pakana na Swalahu-Dini, Nainawa na Ambaar kwa ushirikiano wa jeshi la serikali ya Iraq na Hashdi Sha’abi.