Marjaa dini mkuu ahimiza kua na utaratibu mzuri wa utunzaji wa maji hapa Iraq aidha amehimiza kuishi kwa amani na kuwarejesha wakimbizi katika miji yao pamoja na kuwajengea…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu ametaka kuwe na mkakati mzuri wa utunzaji wa maji hapa Iraq, aidha amehimiza kulinda mshikamano na umoja na kudumisha mapenzi na undugu pamoja na kueneza utamaduni wa kuishi kwa amani kwa tabaka zote za raia wa Iraq, hali kadhalika amehimiza kufanya juhudi za kuwarudisha wakimbizi katika miji yao na kuwajengea pamoja na kuwasaidia kujikimu kimaisha ili kuwapunguzia machungu waliyo nayo.

Hayo aliyasema katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa (5 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (24 Novemba 2017m) iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Sayyid Ahmadi Swafi, ambapo alibainisha mambo mawili:

Jambo la kwanza:

Hakika ni lazima kulinda turathi za taifa, hakuna asiye jua kua taifa letu ni miongoni mwa mataifa ambayo Mwenyezi Mungu ameyatunuku neema na rasili mali nyingi, na miongoni mwa rasili mali zetu ni maji.

Kila mtu anajua maji ndio kila kitu katika uhai, hivyo ni muhimu watu wanao husika na sekta ya maji –kua na mikakati madhubuti- jambo hili walipe umuhimu mkubwa, tupo katika wakati ambao tunapata taarifa za maji zisizo ridhisha katika taifa letu.

Kuna tishio la ukosefu wa maji katika baadhi ya miji wanayo lima na baadhi ya maeneo ya wafugaji, pia kuna baadhi ya miji hawana maji mazuri ya kunywa, hivyo ni muhimu kuwa na mkakati wa wazi kuhusu maji kutokana na unyeti wa swala hili, serikali inatakiwa ilete mkakati wa kutunza maji katika kila mji, wanaweza kutumia serikali za maeneo husika kutengeneza mahodhi ya maji na kutatua tatizo hili, pia lazima kuwe na mkakati wa kulinda vyanzo vya maji, na hili ni jukumu la kila mtu na kila taasisi, kila mtu anatakiwa afanyie kazi swala hili.

Jambo la pili:

Baada ya magaidi wa Daesh kukaribia kuchukua nchi, kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na kutokana na damu tukufu za wapiganaji wetu wa aina zote wamefanikiwa kuzuia hilo, tunamuomba Mwenyezi Mungu adumishe amani na utulivu katika taifa hili, lazima tutafakari vizuri na kuweka misingi ya umoja na mshikamano na kudumisha undugu na mapenzi pamoja na kueneza utamaduni wa kuishi kwa amani na upendo kwa raia wa tabaka zote, hakuna asiyejua umuhimu wa swala hili kwa sasa, na hili ni jukumu la kila mtu.

Kwa upande mwingine, tunatakiwa kuhakikisha wakimbizi wanarudi katika miji yao na wasaidiwe kujengewa nyumba zao kwa kiasi itakavyo wezekana pamoja na kuwasaidia kujikimu kimaisha ili kuwapunguzia machungu waliyo nayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: