Katika kumbukumbu ya kufariki kwa bibi Sukaina bint wa Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Bibi Sukaina mwanamke mwema mtakasifu, alikua mbora wa wanawake wa zama zake, alikua na tabia njema, mwingi wa ibada, anahistoria nzuri, alikua mwingi wa ukarimu, mwenye akili pevu, alipambika na kila zuri.

Ukaribu wake na Maasumina: Ni mjukuu wa Imamu Ali na bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ni mtoto wa Imamu Hussein na dada wa Imamu Zainul-Aabidiin na dada wa Imamu Baaqir (a.s).

Jina na nasaba yake: Sukaina bint Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Mama yake: Rubaab bint Amri-Qais bun Adiy Alkalbiy.

Kuwepo kwake Karbala: Bibi huyu mtukufu (a.s) alikuwepo Karbala na aliona yaliyo tokea Karbala, namna maadui walivyo mzunguka baba yake na watu wa nyumbani kwake na kuanza kuwaua, na aliukumbatia mwili wa baba yake baada ya kuuawa kwake.

Kuchukuliwa kwake pamoja na mateka: Alikua miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) waliochukuliwa mateka pamoja na vichwa vya mashahidi wakapelekwa katika mji wa Kufa, kisha wakatolewa Kufa na kupelekwa Sham, kisha alirudi pamoja na kaka yake Imamu Zainul-Aabidiin (a.s) wakiwa na mateka wengine katika mji wa Madina.

Mapenzi ya Imamu Hussein (a.s) kwake: Imepokewa kua pindi wanawake wa nyumba ya Mtume (a.s) walipo ingizwa kwa Yazidi bun Muawiya, alimuambia Rubaab (mama yake Sukaina): Wewe ndiye ambaye ndani kwako anapo kuwepo Suakaina Hussein alikua anasema:

Hakika mimi naipenda nyumba *** ambayo ndani yake kuna Sukaina na Rubaab.

Nawapenda sana nitatumia mali nyingi *** na wala kufanya hivyo hakuta niumiza.

Kufariki kwake: Alifariki (a.s) mwezi 5 Rabiul-Awwal 117 Hijiriyya, katika mji wa Madina na akazikwa katika makaburi ya Bakii kama ilivyo tajwa katika Shadharaat Dhahabu, na ikanukuliwa na Sayyid Muhsin Amiin katika kitabu chake cha A’ayaan, (Alifariki katika mji wa Madina, siku ya Alkhamisi mwezi tano Rabiul-Awwal mwaka wa 117 Hijiriyya). Ni mashuhuri kua alizikwa katika mji wa Madina.

Miongoni mwa maneno ya washairi kuhusu yeye: Mshairi Yusufu bun Amirah Nakhaii Alkufiy (miongoni mwa maswahaba wa Imamu Swadiq na Imamu Alkadhim (a.s)) anasema:

Na mtumishi wenu Sefu bun Amirah *** hakika mja mtumishi wa Haidari ni Qambar.

Na Sukaina kutokana naye utulivu uliondoka *** pindi alipoanza kuondoka na kubadilika.

Na Ruqayya alikutana na mateso kwa udhaifu wake *** na walimuomba samahani ambayo haijawahi ombwa.

Na Ummu Kulthum alipata upya wake *** hakika mwisho wa machozi yake haujirudii.

Siwezi kumsahau Sukaina na Ruqayya *** walivyo mlilia usiku na mchana.

Amani iwe juu yake bibi mtukufu, siku aliyo zaliwa na siku aliyo fariki na siku atakayo fufuliwa kwa matashi ya Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: