Baada ya kumaliza siku mbili katika vita ya kukomboa kisiwa kikubwa: viongozi wa kikosi cha Abbasi wanabainisha mafanikio waliyo pata hadi sasa…

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa (5 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (24/11/2017m) viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wameeleza mafanikio waliyo pata katika vita inayo endelea chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume wa Mwenyezi Mungu ni mwisho wa mitume) ya kukomboa jangwa kubwa kama ifuatavyo.

 • - Jumla ya aridhi iliyo kombolewa hadi sasa ni kilometa 400.
 • - Kukomboa barabara ya Hadhar – Rawah ambayo ni barabara muhimu kimkakati kwa maadui katika eneo hili.
 • - Kukomboa vijiji vya (Shaikhaan, Shaikha, Burait, Samnu, Al-Bu-Aadil, Talul Muiniy, Khasham, Dhaibaan, Dhayaab pamoja na maghala ya chini ya aridhi).
 • - Kudhibiti magari yaliyo jazwa vilipuzi na kuyalipua chini ya uangalizi.
 • - Kudhibiti nyumba iliyo tegwa mabomu na kuilipua chini ya uangalizi.
 • - Kulipua idadi kubwa ya mabomu yaliyo tegwa aridhini na kusafisha makumi ya kilometa za barabara kwa kutumia mitambo ya kisasa.
 • - Kudhibiti hazina ya siraha zilizo kua zimeandaliwa kwa ajili ya kutumiwa na maadui, hivyo kupata ngawira za siraha na vifaa.
 • - Kudhibiti kituo kukuu cha mawasiliano kilicho kua kinatumiwa na maadui.
 • - Tumepata ngawira ya vifaa vingi vilivyo achwa na maadui waliokimbia.
 • - Kushambulia gari la maadui kwa kutumia ndege za kivita lililokua limebeba wapiganaji na kuua madaesh 15.
 • - Kukomboa uwanja wa ndege wa kivita wa Jiniva na kuanza kutua na kuruka kwa ndege za kivita katika uwanja huo.
 • - Kufungua maeneo salama ya kupita watu wanao kimbia vita.
 • - Kuvamia jangwa la kisiwa kikubwa na kukata mawasiliano ya Daesh na barabara kuu kusini ya mji wa Hadhar jambo ambalo limesaidia vikosi vinavyo pigana kutokea upande wa (Rawah wakielekea katikati ya jangwa kubwa – na wanao pigana kutokea upande wa kisiwa cha China - na wanao pigana kutokea upande wa milima ya Makhuul – na wanao pigana upande wa Talul Baaj – na wanaopigana kutokea upande wa mapandanjia ya Sharqaat).
 • - Hakuna hasara upande wetu: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu.
 • - Mafanikio yote haya yamepatikana ndani ya saa tano tu za mapambano.

Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi zetu wema ambao ndio msingi wa mafanikio haya, na awaponye haraka majeruhi wetu watukufu, na awalinde majemedari wetu ambao baadhi yao wamekwisha kufa na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha ahadi hata kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: