Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu wamtembelea muhadhiri Abdul-Amiri Almansuri kumjulia hali, naye ashukufu kutembelewa na asema kumempunguzia maumivu…

Maoni katika picha
Kutokana na kuwajali wahadhiri wa mimbari ya Hussein na kuwakirimu kutokana na huduma yao ya kuiongoza jamii, na kufuatia fadhila za kutembelea wagonjwa na kuhimizwa jambo hilo na uislamu, ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya miongoni mwa ziara ambazo huwa wanafanya, wamemtembelea Shekh Abdul-Amiri Almansuri katika mkoa mtukufu wa Karbala, kwa ajili ya kumjulia hali na kumpa msaada wa kimanawiyya kutokana na maradhi aliyo pata hivi karibuni.

Shekh Abdul-Amiri Almansuri ni mmoja wa wahadhiri wakubwa katika mkoa wa Karbala, na msomaji wa maqtal ya Imamu Hussein (a.s) asubuhi ya mwezi kumi Muharam katika ukumbi wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Ugeni huo wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), waliongea mambo mbalimbali na Shekh Almansuri kuhusu ziara ya Arubaini na utukufu wa watumishi wa Husseiniyya, na walimuombea apone haraka kwa baraka za Ahlulbait (a.s), na wakampa zawadi za kutabaruku na Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shekh Mansuri alishukuru sana kutembelewa, akasema kua: “Muhadhiri anaye simamishwa (kutoa mihadhara) na Mwenyezi Mungu na kusoma katika mimbari za bwana wa mashahidi (a.s), huwaona watumishi wa Husseiniyya na kazi wanazo fanya kua ni watu bora zaidi kuliko kitu chochote, hakika heri na baraka za Ahlulbait (a.s) kwa wafuasi wao na wapenzi wao hazina hesabu, hakika kunitembelea kwenu leo ni miongoni mwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), mmenipa moyo sana na mmenifurahisha mno, na nimehisi kupata nafuu na maumivu niliyo kua nayo yamepungua, ukiongeza na zawadi nzuri miliyo kuja nayo, bendera ya mwezi wa bani Hashim (a.s), inayo beba ponye na baraka kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.

Kumbuka kua miongoni mwa majukumu ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni kuwatembelea watu muhimu kwa mujibu wa ratiba kama ilivyo pangwa, pamoja na kushiriki katika shughuli za taazia, makongamano na mengineyo miongoni mwa harakati zinazo fanywa na Ataba mbalimbali pamoja na taasisi za serikali na za kiraia na katika kila tukio linalo changia kujenga uhusiano mwema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: