Chuo kikuu cha Ameed chapokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo, na rais wa chuo hicho asisitiza kua kitakua chuo cha mfano kwa kutoa elimu bora…

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza usajili na kukamilisha maandalizi ya kuanza masomo, chuo kikuu cha Ameed chini ya idara ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Juma Mosi (6 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (25 Novemba 2017m) kimeanza kupokea wanafunzi walio kubaliwa kujiunga na chuo hicho wa mwaka wa masomo (2017 – 2018) katika michepuo (vitivo) vitatu (Udaktari, Udaktari wa meno na Uuguzi).

Rais wa chuo profesa Jaasim Marzuki katika neno lake la ukaribisho kwa wanafunzi alibainisha baadhi ya mambo ya kimaadili na kielimu yanayo husu wanafunzi, miongoni mwa aliyo sema ni ulazima wa kufuatilia masomo na kuheshimu kanuni za chuo ili kupata ufaulu unaotakiwa hapa Iraq.

Akasisitiza kua: “Chuo hiki kinatarajia kutoa elimu bora kutokana na misingi kilicho jiwekea na kanuni za kimaadili na kielimu ambazo lazima zifatwe na wanafunzi wa michepuo yote ili kiwe chuo cha kupigiwa mfano kwa kutoa elimu bora”.

Baada ya hapo wanafunzi walikaribishwa katika madarasa, ili wakasalimiane na walimu wao na waanze kutambuana, na kupewa ufafanuzi wa awali kwa kila mchepuo pamoja na kuwapa ratiba za masomo, na aina ya selibasi itakayo fatwa pamofa na kufafanuliwa kuhusu masomo ya nadhariya na vitengo.

Atabatu Abbasiyya tukufu, jioni ya siku ya Juma Tano ijayo inatarajia kufanya hafla kubwa ya ufunguzi rasmi wa kituo hiki cha elimu.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni taasisi ya elimu ambayo ipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimesajiliwa chini ya wizara ya elimu ya juu na utafiti, kinatarajia kutoa elimu bora itakayo pigiwa mfano, kinafuata kanuni na vigezo bora vya kielimu vitakavyo kisaidia kuingia katika orodha ya vyuo vikuu binafsi ambavyo ni bora. Chuo kipo katika mkoa mtukufu wa Karbala, mwanzoni mwa barabara ya Karbala – Najafu, karibu na nguzo namba (1238) kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu namba (07602403019) au unaweza kutuandikia kwenye barua pepe (info@alameed.iq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: