Kikosi cha Abbasi chagundua shehena ya siraha na mabomu kusini ya wilaya ya Hadhar…

Maoni katika picha
Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika opreshen ya (Mtume wa Mwenyezi Mungu ni mwisho wa mitume) ya kukomboa jangwa kubwa linalo unganisha mkoa wa Mosul, Swalahu-Dini na Ambaar, wamegundua shehena kubwa ya siraha na mabomu zilizo kua zikitumiwa na magaidi ya Daesh katika kufanya jinai zao.

Taarifa kutoka katika kikosi hicho zinasema kua; kufuatia msako unao endelea kufanywa na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika miji iliyokua ikidhibitiwa na Daesh, na iliyo kombolewa hivi karibuni na wapiganaji wa kikosi hicho, wamefanikiwa kugundua shehena ya siraha na mabomu pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Jiniva kusini magharibi ya wilaya ya Hadhar ambazo ziliachwa na magaidi wa Daesh walio kimbia mapigano.

Taarifa zinasema kua shehena hiyo ni ya vifaa vya mawasiliano, siraha za kivita ndogo, za kati na kubwa, mabomu ya kutega aridhini, mabomu ya kurushwa kwa mitambo dhidi ya binadamu au vitu, siraha za kushambulia ndege, pamoja na siraha zingine nyingi yakiwemo mabomu ya Haaun pamoja na magari ya kubeba siraha na vifaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: