Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu kwenye chuo kikuu cha Bagdad, viongozi wake wasifu ushiriki huo na kusema kua ni wa pekee…

Maoni katika picha
Viongozi wa chuo kikuu cha Bagdad wamesifu ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu ambayo hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa chuo hicho, na wamesema kua ushiriki wao ni wapekee kutokana na ubora wa bidhaa wanazo onyesha, ambazo zina mchango mkubwa sana wa kumjenga mwanafunzi wa chu kielimu na kitamaduni.

Hayo yalisemwa na makamo wa rais wa chuo profesa Abdulatifu Muhammad ambapo alisema kua, “Tunazishukuru Ataba tukufu kwa ushiriki wao wa pekee katika maonyesho haya, hususan Atabatu Abbasiyya, kwa hakika sisi tunajivunia ushiriki wao, kutokana na nafasi kubwa waliyo nayo katika kusambaza elimu bora ya kidini na kiutamaduni kwa wanafunzi wa vyuo, sisi tunaendelea kushirikiana nao rasmi na hua tunapokea vitabu na machapisho mbalimbali kutoka kwao na kuyagawa kwa wanafunzi, daima tunawaombea mafanikio mema katika kila kitu”.

Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya yaliyo anza Juma Pili (7 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (26 Novemba 2017m) katika korido za maktaba kuu ya chuo, umehusisha sehemu kubwa ya machapisho ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekuja kushiriki na zaidi ya aina 450, nyingi katika hizo zinahusu miongozo ya wanafunzi, pamoja na machapisho mengine ya Ataba kama vile majarida na mengineyo, hali kadhalika idara ya kurepea (kutengeneza) nakala kale ambayo ipo chini ya maktaba ya Ataba tukufu, imeshiriki kwa kuonyesha nakala kale ilizo zirepea katika kituo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: