Utengenezaji wa vifaa tiba wa masafa wafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Iraq: Kitengo cha mawasiliano cha Atabatu Abbasiyya tukufu chafanikiwa kuanzisha mtandao wenye uwezo wa kutengeneza vitaa tiba katika hospitali ya Alkafeel…

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na shirika la kimataifa Jenerali Katrick linalo husika na kutengeneza vifaa tiba muhimu katika hospitali, kwa kutumia watalamu wake na wahandisi wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, waliokua tayali kutumia uzowefu wao wa kigeni na ujuzi wao katika kufanikisha mradi huu, hatimaye kwa mara ya kwanza hapa Iraq imewezekana katika hospitali ya Alkaafeel kutengeneza vifaa tiba kwa kutumia njia ya masafa, kwa kutumia watalamu wa shirika hilo wakiwa hukohuko bila kuja wakati litakapo tokea tatizo lolote, jambo hili litasaidia kuendelea kutoa huduma mfululizo bila kusimama.

Kiongozi wa idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Faras Abbasi Hamza na msimamizi mkuu wa mradi huu amesema kua: “Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha utengenezaji wa vifaa tiba unafanyika kwa usalama na haraka katika ubora mkubwa, na hili ni jambo zuri kwa wagonjwa, vifaa tiba vitatengenezwa kwa kufuata viwango vya kimataifa, kwa kua vifaa tiba tulivyo navyo vina viwango vya kimataifa na mashirika yanayo unda vifaa hivyo yameturahisishia njia za kufanya nao kazi”.

Akongeza kusema kua: “Mtandao maalumu wa kutengenezea vifaa tiba katika hospitali umeonganishwa na mitambo ya Mionzi, mtambo wa kupiga picha maghnatusi, na mtambo wa picha za mionzi (Kamera gama), mtambo wa kupiga picha za mawimbi ya sauti, na mitambo mingine ambayo imeunganishwa na mtandao wa shirika la Jenerali Katrick, na utendaji wake unasimamiwa moja kwa moja na watalamu wake kutoka Marekani na Ufaransa kupitia mtandao maalum wa Intanet wa hospitali ya Alkafeel ambao hauingiliani na mitandao mingine kwa ajili ya usalama zaidi, mtangao huo ni miongoni mwa teknelojia ya (IPSEC) ambao ni mtandao usio ruhusu kuingiliwa na mitandao ya nje, hivyo kua na ulinzi mkubwa zaidi, hii ni mara ya kwanza unatumika hapa Iraq.

Muhandisi Faras akabainisha kua: “Kupitia mtandao huu mtalamu wa shirika tajwa hapo juu anaweza kuingia na kukagua vifaa tiba na kuvifanyia matengenezo kama kuna tatizo, sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama katika vifaa tiba, kwa mujibu wa vigezo vilivyo wekwa na shirika, na ikigundilika ishara yeyote ya uharibifu taarifa hiyo hutumwa moja kwa moja makao makuu nao na hufanya marekebisho, hili ni jambo linalo sababisha uendelevu wa mitambo hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: