Mji wa Samara unashuhudia malaki ya waumini wanao miminika kutoka katika mikoa mbalimbali ya Iraq na nje ya nchi katika malalo ya Imamu Ali Haadi na Hassan Askariyyu (a.s), kufuatia kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Hassan Askariyyu (a.s), kilele cha kumbukumbu hiyo ni mwezi 8 Rabiul-Awwal 1439h, watu walianza kumiminika siku nne kabwa ya tarehe hiyo.
Atabatu Askariyya tukufu imejiandaa kikamilifu kupokea mazuwaru na kuwapa huduma zote muhimu, sambamba na kuimarisha ulinzi katika mkoa wote wa Samara kuzuia tukio lolote la kigaidi linalo weza kuharibu mazingira ya ziara.
Kwa upande mwingine Mawakibu (vikundi) vya kutoa huduma vimeenea kila sehemu kwa ajili ya kutoa chakula, maji na malazi kwa mazuwaru watukufu.
Ziara hii imekua ya aina yake kutokana na kusadifu ushidi mkubwa wanaopata jeshi tukufu pamoja na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh na kufanikiwa kukomboa aridhi iliyokua imetekwa na magaidi hao.