Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wampa taazia Swahibul-Asri wa Zamaan katika kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Hassan Askariyyu (a.s)…

Maoni katika picha
Kuhuisha kumbukumbu ya kuawa kishahidi kwa mwezi wa kumi na moja miongoni mwa miezi ya watu wa nyumba ya Mtume, Imamu Abu Muhammad Hassan bun Ali Askariyyu (a.s), na yaliyo jiri kwa watu wa nyumbani kwake na wapenzi wake akiwemo mwanaye Swahibu Asri wa Zamaan Imamu Hujjat Almuntadhir (a.f), katika siku kama ya leo mwezi nane Rabiul-Awwal mwaka wa 260h, Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza msiba na kupambwa na vitambaa vyeusi vinavyo ashiria huzuni na kuandaa ratiba ya maombolezo kwa ajili ya mnasaba huu mchungu, unao fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ayakuze malipo yako ewe Swahibu Zamaan kutokana na msiba huu mkubwa).

Katika ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imetolewa mihadhara mbalimbali ya kidini, asubuhi na jioni kuhusu msiba huu na nafasi ya Imamu Hassan Askariyyu (a.s) katika kuhifadhi urithi wa uislamu na misingi yake mitukufu pamoja na vitisho alivyo kua anapewa na maadui wa uislamu, na namna alivyo pambana na dhulma ya wafalme wa bani Abbasi kwa kufanya subira.

Hali kadhalika watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu leo asubuhi, wamefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala, wakasikiliza muhadhara ulio tolewa na Shekh Kamali Karbalai kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambaye alizumngumzia mazingira ya nyumba ya Imamu (a.s) na dhulma alizo fanyiwa na watawala wa kipindi chake, majlis ilihitimishwa kwa kaswida za maombolezo.

Kisha wafanya kazi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walifanya matembezi ya pamoja kutoka katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), wakipitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, walipo fika katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlis ya pamoja na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, na wakaimba kaswida zilizo onyesha mapenzi na kushikamana kwao na mwenyendo sahihi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alio upigania Imamu Askariyyu (a.s) hadi akauawa kishahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: