Kuanza kongamano la kielimu la kwanza linalo ongozwa na wanawake wa Ataba mbili tukufu chini ya ujumbe usemao (Upekee wa Karbala na uwajibikaji)…

Maoni katika picha
Jioni ya siku ya Juma Nne (9 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (28 Novemba 2017m) katika ukumbi wa Sayyid Auswiyaa ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu zimeanza program za kongamano la kielimu la wanawake linalo fanyika kwa mara ya kwanza chini ya usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kauli mbiu ya kongamano inasema (Ewe dada yangu naihusia nafsi yako kutenda mema) na ujumbe wake mkuu unasema (Upekee wa Karbala na uwajibikaji), litadumu siku mbili, Juma Nne na Juma Tano, kongamano hili limepata mahudhurio makubwa katika siku ya kwanza, yakiongozwa na kiongozi kutoka Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na kiongozi kutoka Atabatu Abbasiyya, sambamba na idadi kubwa ya viongozi wa vitengo vya wanawake katika Ataba mbili tukufu.

Kikao cha kongamano hili kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ukaibwa wimbo wa taifa ukafuatiwa na wimbo wa Atabatu Husseiniyya tukufu (wito wa aqida), halafu ukafuata ujumbe wa taasisi ya (Waarithu Anmbiyaa lidirasaat tahkasusiyya fi nahdhat Husseiniyya), kisha ukatolewa muhadhara wa kielimu na dokta Ibtisam Madaniy kutoka katika kitivo cha malezi ya msingi katika chuo kikuu cha Kufa, kisha wakaanza kujadili mada (60) za watafiti zilizo pasishwa kujadiliwa kutoka katika jumla ya mada (107) zilizo wasilishwa.

Miongoni mwa malengo makuu ya kongamano hili ni kuonyesha nafasi ya mwanamke katika elimu na athari yake katika kutangaza muhanga wa Imamu Hussein na kufikia malengo ya muhanda huo, pamoja na kuonyesha nafasi yake kifikra na kitamaduni sambamba na nafasi yake katika kurekebisha jamii.

Kikao cha mwisho, kitatacho fanyika kesho siku ya Juma Tano (10 Rabiul-Awwal 1439h) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani Atabatu Abbasiyya tukufu, kitashuhudia kuwasilishwa kwa manufaa yaliyo tokana na kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: